Dawa Moja Maisha Mawili

Episode 2 of 2

Katika maisha yangu yote kama Bwana Mganga, sikuwahi kuona kama ulinzi wangu ulikuwa wa mwisho, mpala leo hii. Dawa moja, yenye nguvu ya kuokoa maisha, ililala kwenye mkebe mdogo wa plastiki mkononi mwangu. Ilionekana kama maji ya kawaida, lakini ndani yake kulikuwa na mfululizo wa maisha ya baadaye—na kifo cha lazima cha mwingine.

Mgonjwa wa kwanza alikuwa amelala kitanda namba 5: Zainabu. Mpenzi wangu wa zamani, ambaye nilimkosea miaka mingi iliyopita. Nilipotimiza ndoto yangu ya kuwa daktari, nikamwacha kwa uchungu na maombi yasiyokusudiwa. Sasa, dunia imemrudishia kwangu mbele ya macho yangu, akiwa mgonjwa mzito wa saratani ya damu. Asilimia 50 ya kupona tu. Ana mtoto mdogo anayemtazama mamake kutoka kwenye mlango wa chumba, macho yake yenye maswali na hofu.

Mgonjwa wa pili alikuwa amelala kitandani namba 8: Bi. Farida, mkunga wa pekee katika hospitali yetu ya mtaa. Mgumu, mwenye huruma, anayezalisha watoto kwa uhodari na upendo. Leo asubuhi alipatwa na homa kali ya malaria ya ubongo baada ya kusaidia kuzalisha mama mmoja mapaja, bila yeye tungempoteza huyo mama na wanae. Ana asilimia 90 ya kupona. Lakini ikiwa atapotea, hospitali nzima itakatika. Kila mwezi, anasaidia kuzaa wastani ya watoto 25. Kila mmoja wa wale watoto anaweza kuwa daktari, mwalimu, au rais wa baadaye. Gharama ya kumpoteza yeye sio pesa tu—ni maisha ya baadaye ya taifa.

Huku nikishika mkebe wa dawa, nilikumbuka maneno ya Zainabu jana usiku: “Rafiki, ulifanya vyema kufuata ndoto zako, hata kama mimi miasha yamenipatia adhabu, lakini nina furaha angalau mwenzangu umefanikiwa, ninachohofia ni maisha ya mwanangu ambaye atabeba msalaba mzito katika umri mdogo. Naomba Mungu angalau anipatie muda wa kumuona anamaliza shule ya msingi.” Machozi yalitoka kwenye macho yake yaliyochoka. Wakati huo huo, Bi. Farida, hata akiwa kwenye hali mbaya, alikuwa akiulizia kwa sauti dhaifu: “Mtoto wa mama yule yuko sawa? Nimesahau kuwaandikia taarifa kwenye kitabu…”

Mazingira ya hospitali yalikuwa magumu: sauti za kujitahidi kupumua, milio ya wagonjwa, na haraka za madaktari wenzangu. Lakini ulimwengu wangu ulizimia. Dawa hii moja ilikuwa kati ya maisha mawili.

Kumpa Zainabu maana yake ni kutoa nafasi ya kurudiana na mpenzi wa zamani, kukomboa dhambi zangu za zamani, na kumpa mtoto wake mamake tena. Lakini mahesabu yanasema asilimia 50 tu. Inaweza kushindikana, na dawa hiyo itapotea bure.

Kumpa Bi. Farida maana yake ni kuokoa maisha ya mama wengi na watoto wao, kudumisha huduma muhimu zaidi hospitalini, na kufanya uchaguzi wa busara zaidi wa kitabibu. Lakini maana yake pia ni kukaa kimya na kuangalia Zainabu akifa, na kujua kuwa nilikuwa na uwezo wa kumwokoa. Yaani kuamua kumuacha njia panda kwa mara nyingine tena, na mara hii huenda hakutakuwa na nafasi ya masahihisho

Nilichukua mshipi wa dawa. Kila tone lilionekana kuwa na uzito wa maisha.

Ama Zainabu, mpenzi wa zamani mwenye asilimia 50 na moyo wa kusamehe? Au Bi. Farida, mkunga mwenye asilimia 90 ambaye ni msingi wa wengine wengi?, Ingawa umri wake ushafikia alasiri.